Zaidi ya karne moja baada ya Wafaransa kuweka reli mashariki mwa nchi ya Ethiopia, njia ya zamani ya usafiri huo bado ni ya lazima kwa biashara na usafiri, licha ya uwepo wa reli ya kisasa, iliyojengwa na Serikali ya China.

Treni ya abiria na mizigo huondoka kwenye kituo cha Dire Dawa majira ya alfajiri, ikifanya safari zake mara mbili kwa wiki, kwa kubeba abiria na mizigo kwenye mabehewa yaliyotengenezwa mwaka 1955, huku yakifanya safari ya saa 12, kwenda kilomita 200 ambazo ni sawa na maili 125 kuelekea mji wa Dewele, uliopo mpakani mwa nchi ya Djibouti.

Treni ya abiria na mizigo inayofanya kazi na kuvuta mabehewa yaliyotengenezwa mwaka 1955. Picha ya Africanews

Abiria hao, huelekea katika eneo hilo kufanya biashara ya mbogamboga, mirungi, vyakula na vitu vingine ambapo hubadilishana bidhaa kwa mchele, sukari, pasta, viungo, mchuzi wa nyanya na mafuta.

Katika safari hii ya leo, inahusisha sehemu pekee inayofanya kazi ya njia ya awali ya kilomita 784, ambayo hapo awali ilikuwa ikitumika kati ya Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia usio na bandari, na Jiji la Djibouti kwenye Ghuba ya Aden.

Tangu mwaka wa 2016, njia ya reli ya kisasa iliyotumia umeme iliyojengwa na China inaunganisha miji mikuu hiyo kwa kutumia safari ya muda wa saa 12 hadi 18.

Njaa, ukame vyayumbisha familia pembe ya Afrika
Uviko yapunguza kasi vita ya Malaria: WHO