Mwimbaji Diamond Platnumz afunguka kuombwa nafasi ya kumsaini msanii Marioo kwenye WCB Wasafi.

Nyota huyo ameweka wazi kuwa amewahi kufuata na mwimbaji Marioo ambaye alimuomba amsaini kwenye label yake kwa kile alichodai kuwa msanii huyo alikuwa tayari kuwa chini ya label hiyo kwa asilimia mia moja.

Kauli hiyo ya Diamond imeibua gumzo zito kwa mashabiki na wadau wa muziki wa bongo fleva kufuatia idadi kubwa ya watu kutokuona sababu za msingi zilizopelekea mwimbaji Marioo kuomba nafasi ya kusainiwa chini ya lebo hiyo, kutokana na ukubwa ambao tayari ameutengeneza na nafasi aliyonayo kwenye kiwanda cha muziki Afrika mashariki.

“Nitawapa stori ambayo watu hawaijui, kabla ya kutoa ‘Bia tamu’ Marioo alikuja nyumbani, tukazungumza alitaka nimsaini, nikamwambia Marioo, nikikutazama naona unafanya vizuri unanafasi nzuri, nahisi kama kukusaini sio kukutendea haki, kwa sababu wewe tayari unafanya vizuri” amesema Diamond.

Aidha Platnumz aliendelea kwa kuweka wazi kuwa alimshauri mwimbaji huyo kuwa kutokana na kuwa yeye na lebo yake WCB hawako katika maelewano mazuri na baadhi ya vyombo vya habari na abaadhi ya wadau, pengine atakapojiunga na lebo hiyo, anaweza kupoteza kupoteza nafasi kadhaa, ikwamo wateja wake kwa kuwa WCB gharama zao za show ziko juu zaidi, pengine haitakuwa rahisi kwake ikiwa atajiunga na familia hiyo.

Diamond na Marioo. Photo/Unkown

“Nilimwambia akatafakari, kwasababu linawezekana likawa na madhara, haijalishi una matatizo gani kama una matatizo njoo ofisini nitakupa hela, tulizungumza vizuri na mdogo wangu Marioo akanielewa dhamia yangu kwake nzuri.” aliongeza

Kauli hizo za Diamond zimeibua sintofahamu na maswali mengi kwa mashabiki wa Marioo, wengi wakihoji, ni kipi kilichompelekea kuhitaji kuwa chini ya WCB licha ya kuwa anaonekana kuweza kusimama na anafanya vizuri licha ya kuwa hayuko chini ya lebo yeyote ya muziki?.

Also read: ‘Sina roho mbaya wananisingizia tu’ – Diamond Platnumz

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 31, 2022
'Sina roho mbaya wananisingizia tu' - Diamond Platnumz