Diamond Platinumz amethibitisha kuwa ndiye msanii wa Afrika Mashariki mwenye ushawishi na anayekubalika zaidi kwenye anga za kimataifa baada ya kupata mualiko wa kuwa mgeni muhimu kwenye kituo cha runinga kikubwa cha Marekani cha E! Entertainment.

Kituo hicho ambacho kinafahamika kwa kuwa kimbilio la mastaa wa Marekani wanaopishana kwa kufanya ‘Talk Shows’ na ‘reality shows’  na vipindi vingine, kimeanza kutangaza kuwa kitakuwa na ugeni maalum wa Diamond Platinumz katika kipindi chake cha E! VIP kitakachoruka Jumapili hii kuanzia saa tatu usiku kwenye channel ya E!,

Diamond E Entertainment

Diamond anakuwa mgeni muhimu kwenye kipindi hicho kipya kilichoanzishwa rasmi Juni 12 mwaka huu kikiilenga kuwagusa wasanii wakubwa wa sehemu mbalimbali za mabara yanayounda dunia.

Tiwa Savage wa Nigeria alikuwa msanii wa kwanza kufungua kipindi hicho, wengine waliopangwa kwenye orodha ukiacha Diamond Platinumz ni Mafikizolo, D’Banj na Cassper Nyovest.

Magufuli: Tutaufanyia Kazi Mchakato wa Katiba
Jamie Vardy Kuendelea Na Leicester City