Kwa mara ya kwanza, Tanzania imeziwasilisha sura mpya za burudani kwenye tuzo kubwa duniani za African Entertainment Awards USA (AEA USA Awards 2016) zilizopangwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu, Newark NJ Marekani.

Sura mpya za Tanzania kwenye tuzo kubwa hizo kubwa za kimataifa ni DJ wa Clouds Fm, DJ D- Ommy ambaye anawania tuzo ya DJ Bora wa Afrika akichuana na wababe wengine wa kuchezea santuli.

CV ya DJ D Ommy na uwezo wake mkubwa wa kuchezea santuli pamoja na namna alivyoweza kuzitangaza kazi zake bora kumemuwezesha kuwa DJ wa kwanza Tanzania kupata mialiko ya kimataifa akilipwa mkwanja mrefu ughaibuni. Mixing zake alizoanza kuzitoa tangu akiwa DJ wa Times Fm zimekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki  na kuwavutia mapromota wengi kufika dau la kumualika nchini kwao.

Tofauti na wengine, DJ D Ommy kwake hii ni tuzo ya kwanza kutajwa kuwania na imekuwa ni tuzo ya kimataifa. Ni kama amenzia juu moja kwa moja.

Sura nyingine mpya kwenye tuzo kubwa za kimataifa ni Mtangazaji wa Clouds Fm na bloger maarufu, Millard Ayo. Blog yake imemuwezesha kutajwa kuwania tuzo ya blogger bora Afrika.

Millard ameweza kuibadili blog yake kuwa chombo cha habari kinachojitosheleza kwa kuwaajiri vijana kadhaa wanaohakikisha habari zote kubwa zinapatikana ndani ya blog hiyo. Umaarufu wake unatokana kwa kiasi kikubwa na uwezo wake mkubwa wa utangazaji na jinsi alivyoweza kukiimarisha kipindi cha ‘Amplifaya’ akijituma zaidi ya umbali aliotarajiwa kwenda.

Millard Ayo

Sura nyingine mpya ni rapa wa kundi la Weusi, Joh Makini ambaye amefanikiwa kutajwa kuwania tuzo ya mwana hip hop bora Afrika (Best Hip Hop Artist) akichuana na visiki vya marapa wakubwa Afrika kama AKA, Wale, Mhd, Rahiz na Jovi.

Memba wa WCB, Harmonize naye ameianza vizuri safari yake ya Muziki baada ya kutajwa kwa mara ya kwanza kwenye tuzo hizo kubwa kuwania tuzo ya msanii bora mpya (Best New Artist) huku mwenzake Raymond akitajwa kuwania tuzo ya kipaji bora kipya (Best New Talent).

Vanessa Mdee (Best Female Single (Vever Ever) na Linah (Best Female Artist of the Year) wamewatoa wasanii wa kike kimasomaso kwa kupenya kuwania tuzo hizo kwenye mabano.

Video ya ‘Achia Body’ ya Ommy Dimpoz imemuwezesha kuwania tuzo ya video bora ya mwaka katika tuzo hizo, akichuana na video nyingine za wasanii wa Afrika ikiwa ni pamoja na ‘Utanipenda’ ya Diamond.

Diamond anaweza kuwa mbabe wa tuzo hizo kwa kutajwa katika vipengele takribani vitano huku wasanii wake Raymond na Harmonize wakitajwa pia kuwania tuzo mbili tofauti. Wakati Harmonize anatajwa kuwania tuzo ya msanii bora mpya, Raymond anatajwa kuwania tuzo ya kipaji bora kipya.

Ali Kiba hakukosa kwenye tuzo hizo akiwakilishwa na collabo yake na Christian Bella ‘Ninagharamia’, huku Yamoto Band wakiwania tuzo ya kundi kali (Hottest Group).

BOFYA HAPA KUWAPIGIA KURA

Video: Mauaji Dallas, Marekani
Majambazi wadaiwa kuteka kijiji kwa saa kadhaa, Polisi wanena