DMX ameshindwa kuizuia furaha yake akiwa katika viunga vya mahakama ya Manhattan na kujikuta akitupia michano kadhaa baada ya jaji kuamuru kuwa hana hatia dhidi ya mashtaka yaliyokuwa nayamkabili.

Rapa huyo mkongwe alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kukwepa kodi kati ya mwaka 2010 na 2015, katika kipindi ambacho alidaiwa kuingiza kiasi cha dola za kimarekani milioni 2.3.

DMX ambaye alishikiliwa katika selo za polisi za Manhattan kabla ya kufikishwa mahakamani wiki iliyopita, alifanya mitindo huru akimsifia mwanasheria maarufu Murray Richman ambaye amewahi kuwatetea na kuwaondoa kwenye mitego ya kisheria Jay Z, Ja Rule ambaye sasa amepewa jina la utani ‘Don’t Worry Murray’.

“We don’t worry with Murray, Get you out of jail in a hurry / When the government try to bury you / You’re good, early!” Alisikika akirap DMX kwa furaha kuhusu uamuzi wake.

Kwa tafsiri isiyo rasmi alieleza kuwa hawana wasiwasi wakiwa Murray, kwamba unaingia jela kwa haraka lakini wakati serikali ikijaribu kukuzika unakuwa sawa mapema tu.

Katika hatua nyingine, DMX aliyeshikiliwa kwenye jengo lenye rumande za polisi za Manhattan ambako mtuhumiwa anayedaiwa kuwa Bosi wa mtandao mkubwa wa dawa za kulevya  nchini Mexico, Joaquin “El Chapo” Guzman anashikiliwa, alitania kuwa alikuwa karibu naye na walipiga porojo.

“Yeah, El Chapo nilikuwa karibu naye sana tu, tulikuwa tunazungumza,” alisema DMX kabla hajawaweka watu sawa kuwa alikuwa anatania. “Jamani alikuwa kule, labda ningeweza kuongea naye.”

El Chapo aliyewahi kutoroka mara mbili katika magereza yenye ulinzi mkali nchini Mexico anashikiliwa nchini Marekani katika rumande maalum yenye ulinzi mkali.  

Video: Lissu agomea kortini..., JPM atangaza kiama kwa wauza mafuta
Magazeti ya Tanzania leo Julai 20, 2017