Saa 24 baada ya kusitishiwa Mkataba wa kuendelea kukinoa kikosi cha Yanga Princess, Kocha Edna Lema ametoa neno la shukurani kwa Uongozi, Wanachama na Mashabiki wa Klabu hiyo.

Edna amesitishiwa Mkataba baada ya kikosi chake kuanza vibaya Ligi Kuu ya Wanawake kwa kufungwa na Fountain Gate kwa kufungwa 1-0 juzi Jumatano (Desemba 07), katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Edna ametumia kurasa za Mitandao ya Kijamii kuandika ujumbe huo wa Shukurani, akiitakia kila la Kheir Yanga Princess ambayo ina kazi kubwa ya kusaka Taji la Ubingwa wa Tanzania msimu huu 2022/23.

Edna ameandika: Kwanza nianze kwa kushukuru viongozi wa Yanga kwa ushirikiano walionipa kwa muda niliokuwa hapa, niwashukuru pia wachezaji wangu kwa mapenzi mliyokuwa nayo kwangu kwa ushirikiano mlionipa.

Niwashukuru mashabiki kwa sapoti yao kubwa kwangu na kwa team kwa ujumla nadiriki kusema Yanga wamenikuza na kunifanya kuwa mkubwa pengine hata ukubwa nisiostahili kwa sababu ni Club kubwa, najua kila shabiki anaitakia mema hii team na anatamani ipate mafanikio, nilijitahidi kufanya kile kilichokuwa ndani ya uwezo wangu lakini kwa sasa inatosha kwa hapa nilipofika mpaka wakati mwingine.

Pengine hii team inahitaji maisha mengine yasiyokuwa na Edna Lema ili iweze kufanikiwa najua pia kuna machache mazuri nimeyafanya mpaka hii team kufikia hapa japo sikufikia malengo.

Hatuwezi kuwa maadui kwa sababu mimi sio sehemu ya Yanga bado mtabaki kuwa familia yangu mimi na viongozi pamoja na mashabiki, niwashukuru tena na tena kwa mapenzi yenu kwangu, najua kuna wanaonipenda sana lakini team kwanza mtu baadae.

Kama kuna tulipokoseana tusameane maisha mengine yaendelee.
‘Daima mbele nyuma mwiko’

Azam FC yatangaza vita na Young Africans
Polisi yatoa huduma za matibabu kwa Wazee