Klabu ya Everton imepanga mikakati ya kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Wales, Thomas Henry Alex “Hal” (Robson-Kanu),  ambaye amekua kivutio katika fainali za Euro 2016 zinazoendelea nchini Ufaransa.

Everton wamepanga kumsajili mshambuliaji huyo, ambaye kwa sasa yupo huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Readinga mbayo ilimtoa kwa mkopo mara mbili katika klabu za Southend United na Swindon Town mwaka 2008 na 2009.

Meneja mpya wa Everton, Ronald Komen ameonyesha nia ya dhati ya kumsajili mshambuliaji huyo, kutokana na dhamira yake ya kutaka kuisuka upya safu yake ya ushambuliaji ambayo huenda ikapata mapungufu katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.

Mshambuliaji kutoka nchini Ublgiji, Romelo Lukaku anahusishwa na mpango wa kuihama klabu hiyo ya Goodson Park, na tayari klabu za Arsenal, Chelsea, Real Madrid na Juventus zinatajwa kuwa katika harakati za kumsajili.

Robson-Kanu mwenye umri wa miaka 27, hajawahi kuzungumza suala lolote kuhusu mustakabli wa soka lake mara baada ya kumalizana na uongozi wa Reading mwishoni mwa msimu uliopita.

Antonio Conte Ahamishia Nguvu Kwa Gonzalo Higuain
Ndoto Za James Rodriguez Kwenda PSG Zayeyuka Rasmi