Klabu ya Everton inafikiria kuvunja dili la kumuuza mshambuliaji wao kutoka nchini Ubelgiji Romelu Lukaku, ambaye anapigiwa chepuo la kurejeshwa Stamford Bridge (Chelsea).

Uongozi wa Everton ambao tayari umeshatangaza dau la Pauni milion 75 kama ada ya Lukaku, umeripotiwa na gazeti la The Daily Mirror kubadili muelekeo na sasa umejipanga kumuongezea mkataba ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni  135,000 kwa juma.

Meneja mpya wa klabu hiyo Ronald Koeman amekua mstari wa mbele kuhakikisha mshambuliaji haondoki Goodison Park, na mara kadhaa ameushaiwshi uongozi kubuni njia ambazo zitafanikisha jambo hilo.

Wakati Koeman akijaribu kubuni mbinu mbali mbali za kumbakisha Lulaku, mpinzani wake meneja wa klabu ya Chelsea Antonio Conte ameendelea kuonyesha nia ya kutaka kumrejesha Lulaku Stamford bridge.

Lukaku aliondoka Chelsea mwaka 2014, baada ua kuonekana hakidhi mahitaji ya aliyekua meneja kwa wakati huo Jose Mourinho, hivyo alishauri mshambuliaji huyo aliyekua kwa mkopo katika klabu ya Everton kuuzwa moja kwa moja.

Rio Ferdinand Amtahadharisha Paul Pogba
Real Madrid Kumpandishia Mshahara Zinedine Zidane