Familia ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, marehemu Wilson Kabwe imekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa imekataa kuwashikirisha viongozi wa Serikali katika mazishi ya ndugu yao.

Kupitia taarifa rasmi ya familia hiyo, imeeleza kuwa haiwezi kuizuia Serikali kushiriki mazishi ya aliyekuwa mtumishi wake na kwamba aliyenukuliwa katika taarifa ya awali sio msemaji wa familia hiyo.

1

Kabwe ambaye alifariki hivi karibuni nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na saratani ya tezi dume pamoja na ini, anatarajiwa kuzikwa Jumatano ijayo kijijini kwao, Mamba, Mpinji wilayani Same.

Chadema: Mtu Pekee wa Kumsaidia Magufulini ni Lowassa
Mashindano ya ‘Big Brother Africa’ yatupwa kapuni

Comments

comments