Klabu ya FAR Rabat inayonolewa na kocha wa zamani wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Sven Vandenbroeck, imethibitisha itacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Wanamsimbazi.

Taarifa iliyowekwa kwenye kurasa za mitandao ya klabu hiyo yenye maskani yake mjini Rabat nchini Morocco, imeonesha FAR Rabat itacheza michezo minne ya kirafiki, huku ikianza na Simba SC.

Mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya miamba hiyo utachezwa kesho Jumamosi (21,08,2021), mjini Casablanca, ambako Simba SC wameweka kambi.

Mchezo huo utawakutanisha kwa mara ya kwanza kiutendaji makocha Didier Gomes na Sven Vanderbroek ambao wote kwa pamoja wanaifahamu uzuri Simba SC.

Simba SC imeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika utakaoanza mwezi Septemba.

Waziri Junior apokea ofa nne
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 20, 2021