Jeshi la polisi nchini Kenya linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha pili kwa tuhuma za kumchoma kisu na kumuua mwanafunzi mwenzake baada ya kugombania ‘flash disk’.

Mwanafunzi huyo wa Shule ya Sekondari Kibera ambaye sasa ni mtuhumiwa wa mauaji ana umri wa miaka 15, na aliyeuawa ana umri wa miaka 19.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, wanafunzi hao walianza kubishana kuhusu nani ni mmliki halali wa flash disk hiyo, ndipo mmoja akachukua kisu na kumchoma rafiki yake.

Mkuu wa Polisi wa eneo la Sarang’ombe, Edwin Otwori ameeleza kuwa mtuhumiwa alijisalimisha katika kituo cha polisi cha Kibra Jumapili jioni, baada ya kufanya tukio hilo Jumamosi.

Alisema baada ya kumhoji, mtuhumiwa alihamishiwa katika Kituo cha Polisi cha Kilimani akisubiri hatua nyingine za kisheria.

Hata hivyo, mama wa mtuhumiwa pia aliingia kwenye majanga ya mwanaye baada ya wananchi wenye hasira kali kuvamia makazi yao na kuchoma moto nyumba waliyokuwa wanaishi.  

Jeshi la polisi limesema linaendelea na upelelezi kuhusu tukio hilo.

Tanzania: Serikali yaagiza uvaaji barakoa, itawapima wakuu wa mikoa
Serikali yawapandisha madaraja walimu 1,135