Waziri wa Kilimo, Profesa. Adolf Mkenda, amewataka wadau wa zao la ndizi nchini ikiwemo wawekezaji kuchangamkia fursa ya kuzalisha kwa wingi zao hilo ambalo kwa sasa limewekewa mkakati wa kuwa zao kubwa la kibiashara.

Profesa Mkenda ameyasema hayo Leo tarehe 25 Septemba 2021 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wakati akifungua mkutano wa wadau wa zao hilo Kanda ya kaskazini ambapo amesema pamoja na wizara hiyo kuthamini na kuyapa kipaumbele mazao mengini lakini pia ndizi ni zao muhimu kibiashara.

Aidha serikali ipo tayari kuwaunga mkono wadau wote ikiwemo wa uwekezaji  na wakulima wakubwa wa zao hilo kutokana na kwamba wizara ya Kilimo imelipa umuhimu mkubwa kwa lengo la kuwa zao la kibiashara, huku akiwahakikishia kuwa serikali itaongeza huduma za ugani ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa mbegu bora kwa kushirikiana na wadau.

“Zao la ndizi ni muhimu kama zao la chakula na Kama matunda lakini kwa namna tunavyo shughulika na kilimo hichi ni tofauti na nchi nyingine ambapo hulilima kama zao la biashara hivyo naombeni wadau mchangamkie frusa hii kwani serikali ina mkakati wa kuhakikisha zao hili linakuwa la biashara” Amesema Profesa Mkenda.

Amesema kuwa, katika nchi nyingine zao hilo limekuwa likizalishwa kwa wingi ambapo kwa mwaka huzalishwa kwa Tani elfu 60 hadi 70 na kuuzwa maeneo mbalimbali Duniani na kuzinufaisha nchi hizo kiuchumi na kwamba wawekezaji wanapaswa kuona fursa hiyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe, ameziagiza Halmashauri za wilaya nchini kujenga vituo vya ukusanyaji wa zao hilo kwa kuwawezesha vijana kwa kuwakopesha asilimia 10 ya mapato inayotengwa.

Naye Mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali ya mbogamboga, Maua na matunda(TAHA), Dkt Jackline Mkindi amesema kuwa lengo la kuwakutanisha wadau hao ni kwa ajili ya kuaandaa mkakati wa pamoja wa kufufua zao la ndizi kitaifa na kimataifa ili kukabiliana na changamoto ya masoko ya zao hilo na kuongeza mnyororo wa thamani.

Rais Samia afanya uteuzi
Habari Picha: Rais samia alivyowasili Nchini