Rais wa Liberia na mchezaji nyota wa zamani wa soka la kimataifa, George Weah ametangaza kuwania tena muhula wa pili kwenye uchaguzi wa mwezi Oktoba 10, 2023.

Weah amesema, “ Wanainchi wenzangu, nitakuja kwenu hivi karibuni kuwaomba mniongeze tena muhula kwa mara ya pili mlionipa miaka sita iliyopita.”

Rais wa Liberia na mchezaji nyota wa zamani wa soka la kimataifa, George Weah.

Aidha, amejitetea mapungufu ya muhula wake wa kwanza akisema, “Nataka niwahakikishie kuwa hali ya taifa letu ni imara. Hali ya taifa letu ni thabiti. Hali ya taifa letu ni ya amani na usalama. Tunakusudia kufanya iendelee hivi.”

Taifa hilo la Afrika magharibi, bado linaendelea kujiweka sawa kutokana na mfululizo wa matukio ya vita vya wenyewe kati ya mwaka wa 1989 na 2003, ambavyo vilisababisha vifo vya watu 250,000.

M23 Wamkimbiza Papa Francis DRC
Afisa wa Polisi afutwa kazi tukio la maauaji ya raia