Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA, Gianni Infantino amebadili kauli aliyoitoa wakati akifanya kampeni za kuwania nafasi ya urais kuhusu ushiriki wa timu za kombe la dunia ambapo aliahidi kuziongeza hadi kufikia 40, lakini kwa mara nyingine ameibuka na kuushangaza ulimwengu.

Infantino ambaye aliingia madarakani mwanzoni mwa mwaka huu, amesema itapendeza zaidi endapo timu shiriki katika fainali hizo zitaongezwa na kufikia 48.

Amesema kama timu zitaongezwa na kufikia idadi hiyo, utaratibu wa michuano hiyo itabadilika ambapo timu 16 zitalazimika kuchujwa katika hatua ya mwanzo na kuziacha nyingine 32 zikiendelea na mashindano kama ilivyo sasa.

Hata hivyo Infantino ambaye ni rais wa nchini Uswiz ameongeza kuwa ushauri huo alioupendekeza utawasilishwa katika kikao cha bodi ya FIFA kitakachofanyika mwezi Januari mwaka 2017.

”Haya ni mawazo ya kupata suluhisho la uhahika, tutayajadili mwezi huu na kufahamu nini cha kufanya mwaka 2017,” alisema Infantino.

Infantino aliingia madarakani kuliongoza shirikisho la soka duniani FIFA mwezi Februari baada ya kujiuzulu kwa Sepp Blatter.

Tyson Fury Amkacha Rasmi Wladmir Klitschko
Modric, Lovren, Rakitic Kuzikosa Kosovo, Finland