Meneja mpya wa klabu ya Man City, Pep Guardiola ametoa maelekezo kwa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Txiki Begiristain, kuhusu beki wa kati Vincent Kompany ambaye hatokuwa sehemu ya mipango yake atakapotua klabuni hapo mwezi June mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la The Sun, zinaeleza kwamba Pep Guardiola amekua akitoa maelekezo hayo kwa lengo la kuanza kukifuma na kukijenga upya kikosi cha Man City.

Pep ametoa agizo hilo, kwa kuamini Kompany ambaye ni beki kutoka nchini Ubelgiji, hatoweza kuhimili mipango yake kutokana na mapungufu aliyoyaona tangu alipoanza kumfuatilia msimu huu ambapo amekuwa akiumia mara kwa mara.

Meneja huyo ambaye atamalizana na FC Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu, amependekeza kusajiliwa kwa beki wa kati wa klabu ya Athletic Bilbao ya nchini Hispania, Aymeric Laporte kama mbadala wa Kompany.

Beki huyo ambaye yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa chini ya umri wa miaka 21, anaaminiwa na Pep Guardiola atatosha katika mikakati ya kupeleka heshima huko Etihad Stadium, kuanzia msimu ujao.

Wakati agizo hilo likitoka, Kompany kwa sasa anauguza jeraha ya kiazi cha mguu alilolipata wakati wa mchezo wa mkondo wa pili wa ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora, dhidi ya Dynamo Kyiv.

Hata hivyo beki huyo mwenye umri wa miaka 29, bado anaendelea kukumbukwa kwa makubwa aliyowahi kuitendea Man City hadi kufikia hatua ya kutajwa katika kikosi bora cha wachezaji wa ligi ya nchini England kwa mwaka 2011, 2012 na 2014.

Kwa msimu huu Kompany amecheza michezo 12 ya ligi, kutokana kajeraha yanyomuandama mara kwa mara.

Watanzania Wachomoza Kwenye Orodha Ya CAF
Ajali: Mtangazaji wa TV aonesha sehemu za siri bahati mbaya akiwa ‘Live’ hewani (picha)