Watawala wa kijeshi nchini Guinea jana wameondoa uwezekano wa kumruhusu rais wa zamani anaeshikiliwa Alpha Conde kwenda uhamishoni, na kusema mchakato wa mpito kuelekea utawala wa raia utafanyika kulingana na matakwa ya raia wa nchi hiyo.

Msemaji wa kiongozi wa mapinduzi Mamady Doumbouya ameuambia ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS unaozuru nchini humo kwamba ni muhimu kwa Jumuiya hiyo kusikiliza matarajio halali ya watu wa Guinea na kwamba ipo haja ya kutorudia makosa ya zamani.

Taarifa ya baraza la uongozi huo, imetolewa katika kukaidi shinikizo la kimataifa la kuachiwa huru Conde na kuwasilisha ratiba ya miezi sita ya kuandaliwa kwa uchaguzi, baada ya mapinduzi ya Septemba 5 kuibua ukosoaji wa kimataifa.

Hata hivyo katika mkutano wa kwanza wa baraza hilo la uongozi na wanahabari kuhusu muda wa mwisho wa miezi sita wa kuandaliwa kwa uchaguzi.

Mbunge wa jimbo la Namtumbo apata ajali
Rais wa Zambia awafuta kazi vigogo