Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Gutteres, amesema kuwa anapenda sana mwaka 2017, uwe wa amani.

Gutteres amesema hayo ikiwa ni siku yake ya kwanza kuanza kazi rasmi kama Katibu Mkuu wa UN, baada ya Ban Ki Moon kumaliza muda wake. aidha ameongeza kuwa malengo yake makubwa ni kuwasaidia mamilioni ya watu walioathiriwa na migogoro ya kivita.

Aidha amesema kuwa  maendeleo hayawezi kupatikana pasipo na amani, hivyo ni wakati wa kila mtu kuhubiri amani.

Hata hivyo, kumeanza kuibuka kwa taarifa mbalimbali kuhusiana na changamoto lukuki zinazomkabili Katibu Mkuu huyo, ikwemo migogoro ya nchi za kiarabu, pia mapokeo mabaya dhidi ya UN kwa rais mteule wa Marekani, Donald Trump ambaye alitoa matamshi ya kuikashifu na kuipuuza kazi ya Umoja wa Mataifa kwa kudai wanapiga porojo.

Ndikilo awapa siku 30 wafugaji kuondoa mifugo yao
Pofessor Jay afunga mwaka kwa kumvalisha pete mama watoto wake