Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amezindua Mradi wa kuimarisha Afya, Ustawi na ulinzi kwa watoto na vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi, USAID Kizazi hodari.

Akizungumza na washiriki wakatia wa hafla ya uzinduzi huo jijini Dodoma, Waziri Gwajima amewataka Watekelezaji wa mradi huo kutoa elimu sahihi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto na kuendeleza programu za kuwaandaa wavulana kuja kuwa wanaume bora.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima.

Amesema, “Mimi binafsi nitakuwa mstari wa mbele kwenda kwenye maeneo ya utekelezaji kuona maendeleo ya mradi huu. Aidha, katika kuboresha huduma za afya na ustawi wa jamii kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi pamoja na walezi wao, Wizara inaona vema afua hizo ziwekwe” amesema Dkt. Gwajima.

Aidha, Waziri Gwajima pia ameongeza kuwa, ili kuendeleza utekelezaji wa shughuli za usimamizi wa mashauri ya watoto inatakiwa kutoa huduma kamilifu na endelevu na kuimarisha mifumo ya huduma za ulinzi na usalama wa Watoto katika jamii pamoja na kushirikiana na Mikoa na halmashauri kufanya ufuatiliaji na kusimamia ubora wa takwimu.

Mradi wa umeme JNHPP mbioni kukamilika
PICHA: SSC Napoli waishangaza dunia