Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela Lubinga amesema kuwa katika awamu hii ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli hakuna fisadi wala mla rushwa atakayepona.

Ameyasema hayo wakati akitoa mada kwenye darasa la itikadi kwaajili ya vijana wa vyuo vikuu mkoani Dodoma ambapo amesema kuwa kila aliyeiba mali ya umma ni lazima atashughulikiwa ikiwa ni pamoja na kutaifishwa mali zote alizoiba.

“Serikali imejipanga kurejesha mali zote zilizoibiwa hivyo, popote walipo watashughulikiwa na hakuna atakayepona katika vita hii, Rais anapambana na wezi wa madini lakini kuna baadhi ya wananchi badala ya kumuunga mkono wao wanaanza madai kuwa nchi itashtakiwa,”amesema Lubinga.

Hata hivyo, Lubinga amewataka vijana kutoruhusu adui ndani ya chama hicho kwakuwa Serikali ya CCM wapo baadhi ya watumishi ambao hawatendi haki.

 

El Hadji Diouf: Mimi sio mtu mbaya, Ulaya walinionea
Remy Ma akomesha utawala wa Nick Minaj kwenye tuzo za BET