Baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Singida Big Stars jana Jumatano (Novemba 23), Kikosi cha KMC FC kinakabiliwa na changamoto ya wachezaji sita tegemeo ambao ni majeruhi.

Wachezaji hao ni Hance Masound aliumia akiwa kwenye mchezo wa jana uliopigwa Uwanja wa Liti mkoani Singida, hali iliyopelekea kushindwa kuendelea na alilazimika kukimbizwa Hospitali na gari la wagonjwa (Ambulance).

Wengine ambao walishindwa kuendelea na mchezo huo ni Ibrahim Ame, Baraka Majogoro.
Wachezaji hao watatu wanaungana na wengine waliokua majeruhi kabla ya kuivaa Singida Big Stars ambao ni Kelvin Kijili, Awesu Ally Awesu pamoja na Emmanuel Mvuyekure.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino wa KMC FC Christina Mwagala amesema: “Kwa sasa tunakabiliwa na changamoto kubwa ya wachezaji wenye majeraha, na ukiangalia kwenye Timu kila mchezaji anamchango mkubwa pindi anapopewa majukumu na kocha, hivyo nikipindi kigumu lakini tutajitahidi kadiri tuwesavyo ili kufanya vizuri kwenye michezo inayokuja.”

Katika hatua nyingine KMC FC imerejea Jijini Dar es salaam leo Alhamis (Novemba 24) majira ya alfajiri, ikitokea mkoani Singida na kesho Ijumaa (Novemba 25) itaanza kufanya maandalizi kuelekea katika mchezo unaokuja dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Novemba 28 katika uwanja wa Uhuru Jijini hapa.

Lionel Messi: Tulizidiwa, tusilete visingizio
Mlipuko homa ya Dengue wauwa 26