Wahehe ni moja kati ya makabila yaliyotokea kwenye bonde la mto Rufiji. Hili ni kabila linalopatikana Tanzania ambalo kiasili linaishi katika wilaya za Mkoa wa Iringa, Iringa mjini, Iringa vijijini, Kilolo na Mafinga.

Wahehe pia wanatajwa kuwa ni kati ya makabila maarufu kwa jinsi walivyopambana na Wajerumani walioteka maeneo yao, katika pigano la Lugalo mwaka 1891. Na kiongozi wao alikuwa Chifu Mkwawa.

Lugha ya Wahehe ni Kihehe na imegawanyika katika matamshi tofauti tofauti kutokana na maneno yanayozungumza na lugha hiyo inafanana na lugha ya Kibena iliyopo mkoani Njombe, pia na lugha ya Kisangu iliyopo mkoani Mbeya.

 

Video: DC Mjema azindua kampeni ya upandaji miti
Waziri Mkuu wa Ethiopia kutua nchini kesho