Serikali imeshauriwa kutunga sheria mahususi itakayowabana wanaofanya ukatili dhidi mtoto majumbani, licha ya kosa hilo kuwa miongoni mwa makosa ya jinai.

Ushauri huo umetolewa na Mwanasheria Zakia Msangi, kutoka Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF), alipozungumza na Dar24 Media, kutokana na makosa ya ukatili dhidi ya mtoto kuendelea kuongezeka, amesema ni vema pia kuwe na Mahakama ya kifamilia itakayosaidia kuendesha kesi za makosa hayo kwa haraka zaidi na mtu kupata haki zake.

Msangi amesema ni vema na muhimu elimu kwa jamii iendelee kutolewa juu ya haki za mtoto ambayo isaidia jamii kuelewa jinsi gani ya kumlinda mtoto.

Ameongeza kuwa ni vema pia serikali ingeangalia ni kwa namna gani mitaala ya elimu shule ya msingi kuongezewa somo linalohusisha elimu za ukatili wa kijinsia.

Msangi ametaja baadhi ya sababu zinazosababisha ukatili wa kijinsia kwa mtoto kuendelea katika jamii zinazotuzunguka ni pamoja na wazazi kukimbia majukumu yao ametolea mfano suala la mzazi kumpeleka mtoto shule za bweni na kusema amebanwa na majukumu, pia ametaja wazazi kuwachia madada wa kazi kuwa walezi wa wototo na kukosa muda wa kuzungumza na watoto.

Pia ametaja sababu ya watoto kuangalia vipindi visivyo na maadili mazuri inachangia kukuza ukatili wa kijinsia akitolea mfano watoto kuangalia vipindi vya maigizo ya mapenzi ya jinsia moja na kumfanya mtoto kutaka kujaribu tendo hilo.

Kisa Simba Queens, meneja asusa
Nikki wa Pili kuwa mkuu wa Wilaya, Rais Samia kaona hili