Hillary Clinton amejitangazia ushindi katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic nchini Marekani, baada ya kupata ushindi katika jimbo la New Jersey.

Kufuatia ushindi huo aliojihakikishia, Hillary Clinton atakuwa ameweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kuteuliwa na chama chochote kikuu nchini humo kugombea nafasi hiyo.

“Natamani mama yangu angekuwa hapa aone mwanae ametengeneza historia ya kuwa mwanamke anayegombea urais kwa tiketi ya Democratic,” alisema Bi. Clinton.

Bi. Clinton amempongeza mpinzani wake Bernie Sanders kwa kuendesha kampeni za kistaaarabu ingawa bado hajakubali kushindwa na anatarajia kuwashawishi wajumbe kumuunga mkono katika jimbo la California.

Katika hotuba yake kwa wanachama Democratic, Hillary Clinton amemkosoa mgombea wa Republican, Donald Trump akieleza kuwa hafai kuwa Rais. Alisema kuwa kauli zake zimelenga katika kuwavuguruga Wamarekani na kuwarudisha nyuma.

“Anaposema ‘ngoja tuitengeneze Marekani yenye nguvu kubwa tena, anamaanisha ‘hebu turudi nyuma’,” alisema.

Kenya: Tumbili azima umeme Nchi Nzima
Bajeti ya Kwanza ya Magufuli kusomwa leo, Ukawa waahidi kutoa vipande na kususa