Kampuni ya bahati nasibu inayodhamini ligi kuu ya soka nchini Kenya, imesaini mkataba wa kuidhamini  klabu ya Hull City itakayoshiriki ligi kuu ya England mdimu wa 2016/17.

Kampuni hiyo ya SportPesa, ambayo huandaa michezo ya kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali, imeingia mkataba na klabu hiyo ya KC Stadium wa miaka mitatu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye klabu hiyo, udhamini wa SportPesa umekua ni wa gharama kubwa, na haujawahi kutokea klabuni hapo katika kwa miaka 112 ya historia ya The Tigger.

Klabu ya Hull City ilifanikiwa kurejea kwenye ligi ya soka England, baada ya kuwa sehemu ya timu tatu zilizomaliza katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi daraja la kwanza nchini humo msimu uliopita.

Hull City watafungua msimu kwa kupapatuana na mabingwa watetezi Leicester City.

Kabla ya kampuni ya SportPesa, klabu ya Hull City ilikuwa ikidhaminiwa na kituo cha burudani cha Flamingo Land kilichopo nchini England.

Waziri Mkuu Kuhamia Dodoma Septemba Mwaka Huu
Nolito: Nimeikataa FC Barcelona Kwa Sababu Ya Pep Guardiola