Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mwenyekiti Mpya wa Mfuko wa Washirika Wafadhili wa Elimu Duniani (GPE) Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameahidi kwa Mtngulizi wake Julia Gillard kuwa wataendelea kuimarisha Taasisi hiyo ya GPE ili kusaidia mabadiliko chanya katika Elimu

Ameyasema hayo wakati akihutubia katika Mkutano Mkuu wa Mfuko wa Washirika Wafadhili wa Elimu Duniani unaofanyika London Uingereza.

Rais Msataafu wa Awamu ya Nne na Mwenyekiti Mpya wa Mfuko wa Washirika Wafadhili wa Elimu Duniani (GPE) Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kwenye Mkutano wa Taasisi ya GPE,
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako alipata fursa ya kuhutubia wajumbe wa mkutano huo ambapo ameelezea maboresho mbalimbali yanayofanywa na serikali katika sekta ya elimu nchini.
Picha za viongozi, Rais Uhuru Kenyata wa Kenya, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ,waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Simai Mohammed Said na Viongozi kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Mfuko wa Washirika Wafadhili wa Elimu Duniani ( GPE) unaofanyika London ,Uingereza

Tatizo la maji Mkoa wa Pwani kubaki historia
Rais Mwinyi afanya uteuzi