Kocha kutoka nchini Ufaransa Herve Renard atakutana na waajiri wake wa zamani timu ya taifa ya Ivory Coast katika fainali za Afrika za mwaka 2017, baada ya shirikisho la soka barani humo (CAF) kukamilisha zoezi la upangaji wa makundi usiku wa kuamkia hii leo.

Renard aliiwezesha Ivory Coast kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka 2015 katika fainali zilizofanyika Equatorial Guinea (Guinea Ya Ikweta), kwa kuifunga timu ya Ghana kwa changamoto ya mikwaju ya penati 9-8.

Kwa sasa kocha huyo ambaye pia aliwahi kuisaidia Zambia kutwaa ubingwa wa Afrika katika fainali za mwaka 2012, anakinoa kikosi cha Morocco.

Morocco na Ivory Coast wamepangwa katika kundi C sambamba na mataifa ya Jamuhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo pamoja na Togo.

Katika fainali hizo wenyeji Gabon watafungua kwa kucheza dhidi ya Guinea-Bissau katika uwanja wa l’Amitié, mjini Libreville.

Fainali za Afrika mwaka 2017 zimepangwa kuanza Januari 14, na kufikia tamati Februari 5.

Muonekano wa timu na makundi ya AFCON 2017

Kundi A

Gabon, Burkina Faso, Cameroon na Guinea Bissau

Kundi B

Algeria, Tunisia, Senegal na Zimbabwe

Kundi C

Ivory Coast, DR Kongo, Morocco na Togo

Kundi D

Ghana, Mali, Misri na Uganda

Ulikua Usiku Wa Kibabe, Miamba Ya Ulaya Yaunguruma
Lil Ommy wa Times FM kupiga kambi Afrika Kusini kwa tuzo za MTV