Mke wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Janeth Magufuli  aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ameruhusiwa kuondoka hospitalini hapo mara baada ya afya yake kuimarika na kurejea nyumbani, Mama Janeth alilazwa hospitalini hapo Jumatano baada ya kuugua ghafla na kupoteza fahamu.

“Namshukuru sana Mungu kwamba afya yangu imeimarika, pia napenda kuwashukuru Madaktari na Wauguzi, nimepata huduma nzuri sana maana siku nilipoletwa hapa nilikuwa sina fahamu na hali yangu ilikuwa mbaya lakini mmenipigania na leo narudi nyumbani nikiwa na afya imara,” alisema Mama Janeth.

Aidha,amewashukuru  Watanzania wote kwa kumuombea na kuwahakikishia kuwa yupo vizuri  na madaktari wamemruhusu arudi nyumbani ambako atamalizia matibabu yake.

Hata hivyo, Rais Magufuli alikwenda kumjulia hali mkewe,na kupata nafasi ya kuonana na wagonjwa wengine waliolazwa katika wodi ya Sewa Haji na kumshukuru kwa jitihada alizozifanya za kuboresha hospitali ya taifa ya Muhimbili na kubainisha kuwa licha ya kuboreshwa kwa mazingira ya hospitali, pia wanapata huduma nzuri kutoka kwa madaktari na wauguzi.

Wanafunzi vyuo vikuu waaswa kuepuka migomo na maandamano
Video: Waziri Mwakyembe amlilia Samuel Sitta Bungeni