Ikitajwa historia ya muziki wa hip hop Duniani, kwa namna yeyote hayatoachwa kuorodheshwa majina ya nyota wawili wa muda wote, 2 Pac na Notorious B.I.G miongoni mwa wasanii wenye historia ya kusisimua inayoaminika kuwa na nguvu ya kudumu kwa vizazi na vizazi vya wafuasi wa muziki wa hip hop duniani.

Washiriki wawili wa muziki wa Hip Hop waliofanya vizuri zaidi, 2Pac na The Notorious B.I.G. vifo vyao vilifuatana kwa tofauti ya miezi sita ambapo wote kwa pamoja walifariki dunia kwa kuuawa mwishoni mwa miaka ya 90.

2Pac alipigwa risasi na kuuawa huko Las Vegas mnamo Septemba 1996, wakati Biggie alipigwa risasi huko Los Angeles mnamo Machi 1997.

Wakati huo wote walikuwa katika kilele cha mafaniko ya kimuziki wakiwa na kundi kubwa la wafuasi duniani kote na kupelekea vifo vyao na kuacha jeraha na pengo kubwa katika jamii ya Hip Hop ambalo haikuwahi kutokea kuaminika kuwa atapatikana mtu au watu wa kuliziba pengo hilo kamwe.

Lakini kwa mujibu wa rapa P Diddy, yeye ameweka mtazamo wake wazi ikiwa ni pamoja nakubainisha kuwa pengo la wawili hao tayari limepata mtu sahihi aliyeliziba kwa kuichukua nafasi ya mahasimu hao ambapo amemtaja rapa Jay Z kuwa mtu pekee aliyeweza kuvivaa viatu vya 2pac na B.IG.

Ni wakati wa mazungumzo ya hivi majuzi kupitia Twitter Space, wakati wa shamrashamra za kuadhimisha miaka 50 ya kuzaliwa kwa marehemu Biggie, ambapo Jay Z alikuwa akizungumzia pengo ambalo 2Pac na Biggie waliliacha.

“Kuhusu Big na ‘Pac na kusonga mbele hiyo ilinifanya kuwa mwanafunzi wa mchezo, kupenda mchezo na kupenda utamaduni na kutaka kusukuma utamaduni mbele, Hiyo ndiyo changamoto ambayo nilikuwa nikikabiliana nayo”

Diddy akajibu, “Bro, umevivaa viatu vyao. Umeingia na hakika tunashukuru, Hakika ulikuja, na najua ni kiasi gani Big alimtazama Jay. Yaani ilibidi uingie kwenye viatu vya watu hao wawili, Hov alikuwa anakuja, lakini ilikuwa ni kama Pac na Biggie walikuwa wakubwa sana, na kwa hivyo baada ya yote hayo. nadhani Hov aliendeleza sanaa yake na kuchukua mahali walipokuwa na kuipeleka sanaa hii juu zaidi.”

Laiti kama rapa Notorius B.I.G angekuwa hai mpaka mwaka huu wa 2022, angefikisha umri wa miaka 50 Jumamosi ya juma lililopita (Mei 21).

Katika hafla za kusherehekea kumbukizi za siku ya kuzaliwa kwa marehemu B.I.G, Jengo mashuhuri la Empire State Building huko Manhattan lilipambwa kwa kuwashwa kwa mataa ya rangi nyekundu na nyeupe kama ishara ya heshima ya marehemu rapa huyo huku taswira ya taji ikizunguka mlingoti wa jengo hilo, ikitumika kama ukumbusho wa hadhi yake ya “Mfalme wa New York”.

Katika mtaa Biggie huko Brooklyn, Kituo cha Barclays kilitoa taswira ya video ya baadhi ya nyimbo zake za kitamaduni kwenye onyesho la oculus juu kabisa ya lango la uwanja. MTA pia ilitoa toleo dogo la Biggie MetroCard katika vituo vitatu tofauti huko Brooklyn nchini Marekani.

Rais awataka raia kupambana na hali zao
Sarakasi na Vilio vyaibuka Bungeni