Oktoba 14, 2016 Tanzania imeadhimisha miaka 17 tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere afariki dunia. Mchango wa Baba wa Taifa ulikuwa mkubwa sana wakati wa uhai wake, si Tanzania tu bali hata nchi za Afrika na nje ya Afrika kama China iliyokuwa ikiwakilishwa na Taiwan katika Umoja wa Mataifa(UN) na kuifanya ianze kujulikana duniani hadi sasa imekuwa ‘second financial power’ ya dunia na pia ni ‘super power’.

1. Alipigania uhuru wa Tanganyia kutoka kwa wakoloni wa kiingereza mwaka 1961 Tanganyika ikapata uhuru wake kutoka kwa gavana wa mwisho wa Tanganinyika SIR RICHARD TURNBULL.

2. Mwaka 1964 aliunda rasmi jeshi la wananchi wa Tanzania ( JWTZ/ TPDF) na kumteua CDF wa kwanza mtanzania major Gerneral Mirisho Sarakikya.

3. Mwaka huo huo 1964 alifanya muungano na Zanzibar na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwakubaliano na marehemu Abeid Aman Karume rais wa kwanza wa Zanzibar na kuzaliwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayodumu hadi sasa.

4. Mwalimu aliondoa dhana mbovu ya ukabila, udini, ubaguzi wa rangi ya nchi yaani hakupenda kuwabagua wahindi, waarabu na machotara wa aina zote hapa nchini wote alituthamini sawasawa bila ya kujali uzawa. Mwalimu alimthamini mtanzania yeyote mwenye fikra za maana katika kutoa mchango wa kuliendeleza Taifa.

5. Mwalimu katika utawala wake alihakikisha kuwa watanzania asilimia kubwa hawapishani sana kipato chao pia alidhibiti rushwa kwa asilimia 96 wakati wa utawala wake viongozi wengi na wananchi wengi walikuwa wanaogopa kutoa na kupokea rushwa.

6. Watanzania wengi walifaidika na sera za kupata elimu bure na huduma za afya bure bila ya kujali tabaka, aliwathamini watanzania wote.

7. Mwalimu katika utawala wake alijenga viwanda kama friendship textiles, morogoro shoe company, bora shoes, sungura textiles, Tanzania Portland cement co. mwanza textiles, kiwanda cha mbolea Tanga, Tanzania sisal estates. Tanganyika Packers co, UFI, general tyre, viwanda vya sukari, viwanda vya majani ya chai ( Tanzania tea blenders) viwanda vya TWICO, STAMICO, TAMCO, viwanda vya pamba, viwanda vya kubangua korosho, National Byciycles, viwanda vya ngozi na mashirika mengine ya umma kama NBC, ATC, RELI, BIMA N.K

8. Aliviunganisha vyama vya Tanu na Afro – Shiraz na kuzaliwa CCM mwaka 1977 ambayo bado imeshika hatamu ya utawala wan chi hadi sasa.

9. Mwalimu Nyerere ndiye aliyewaingiza wachina katika umoja wa mataifa miaka ya sabini mwanzoni, wakati huo balozi wa Tanzania UN alikuwa Salim Ahmed Salim, Mwalimu alimwagiza Salim kuwa awaulize UN kwa nini ‘The people’s Republic of China’ inawakilishwa na Taiwan. Wakati huo Taiwan ilikuwa na jumla ya watu million 18 na China mainland walikuwa million 800, hivyo ikabidi UN waamue kupiga kura ambayo ilifanya china wachaguliwe kuiwakilisha Taiwan katika UN. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuifanya China ianze kujulikana duniani hadi sasa imekuwa second financial power ya dunia na pia ni super power.

10. Amevunja record ya nchi za Afrika kwa kuweza kupigana na nchi kubwa kama Uganda, na kuweza kuiteka nchi nzima na kuwaweka viongozi aliowataka yeye ( Ysuf Lule na Godfrey Binaisa) yeye akiwa kama amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Tanzania na majeshi yake aliyaondoa Uganda kwa hiari yake. Haijatokea katika historia ya Afrika nchi yeyote kufanya hivyo Tanzania ni ya kwanza.

11. Alimsaidia Rais Albert Rene wa Seychelles kurudi madarakani baada ya kupinduliwa na James Mancham, JWTZ iliingia pale mahe Seychelles majira ya jioni na ndege za kijeshi za JWTZ aina ya Buffalo zikiwa na askari / commando waliokwenda kuivamia Ikulu ya nchi hiyo na kufanya mapambano makali ya muda mfupi na kumuondoa James Mancham na askari wake wa kukodi walioikalia Ikulu hiyo kwa muda mfupi, JWTZ ilikaa kwa siku chache na kurudi Tanzania salama.

12. Mwalimu ndiye alieongoza mapambano ya kuzikomboa nchi zote za kusini mwa Afrika zikiwemo Mozambique, Angola, Southem Rhodesia – Zimbwabwe. Namibia Afrika Kusini. Alitumia kila aina ya mbinu kuhakikisha kuwa ushindi unapatikana kwa mataifa hayo, na mwenyezi Mungu alimwangazia akaibuka na ushindi dhidi ya tawala dhalimu hizo.

13. Kifo cha Mwalimu ni pigo kubwa kwa watanzania wote kwani imekuwa ni sawa na kumpoteza baba ndani ya nyumba, kwani Mwalimu alipokuwa hai alikuwa akifuatilia kwa makini mwenendo wa nchi na hasa viongozi na alikuwa na uwezo wa kuwakemea wanapokwenda kinyume na maslahi ya Taifa.

14. Mwalimu Nyerere alikuwa muadilifu wa mali za umma hakuwa na tamaa ya kuzifuja rasilimali za Taifa pia hakuwa mfujaji wa fedha za serikali, aliishi maisha ya kawaida kwa muda wote wa miaka 24 aliokaa Ikulu kama rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

15. Mwalimu Nyerere Alikuwa mcheshi na mwenye kupenda kuwasikiliza wasomi na hata wasiokuwa wasomi pia alipenda sana kuongea na wazee waliomzidi umri kupata mchango wao wa mwelekeo wa nchi.

16. Mwalimu Nyerere Alkuwa kiongozi mwenye huruma sana kiasi kwamba aliweza kuwasamehe watu waliokuwa na mipango ya kutaka kuiangusha serikali yake na kumwaga damu ya wananchi wasiyo kuwa na hatia, matukio hayo yalitokea miaka ya 1971 – 1974 N.K Maofisa wote wa jeshi walioshiriki katika hilo kisheria walitakiwa kupigwa risari hadharani (firing squard) Lakini mwalimu aliwasamehe adhabu hiyo ya kifo na badala yake wengine walitumikia vifungo na wengine wakapewa kazi uraiani kitendo ambacho kilikuwa ni cha ucha Mungu.

17. Kifo chake pia kilitoa uthibitisho kuwa alikuwa kipenzi cha watanzania wote kwani nchi nzima ilionyesha majonzi ya uchungu.

18. Kifo chake kilivunja rekodi ya Maraisi wa Afrika ambao waliifia ulaya, Mwl. Nyerere mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa amefariki huko London UK kwenye hospitali ya Thomas ( ST. THOMAS HOSPITAL) Mwl. Alipewa heshima ya hali ya juu na ufalme wa waingereza kwa kupewa heshima zote zinazostahili. Pia hata misa zake ziliombewa katika makanisa ya heshima ya kiingereza.

Maiti yake na jeneza lake lilishughulikiwa kwa heshima zote za kiingereza kwa viongozi wote wanaoheshimika.

Serikali ya wingereza walikuwa tayari wameishatoa ndege bure ya kusafirisha mwili hadi Tanzania, pia South African Airways na wao pia walitoa ndege ya kusafirisha mwili wa Mwl bure hadi Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania chini ya Rais Benjamin Mkapa ilishauriwa kuwa mwili wa Mwl. usisafirishwe na waingereza wala South African Airways ambayo marubani wake ni wazungu, waliokuwa makaburu ambao mwalimu alikuwa adui yao mkubwa.

Hivyo Serikali ya Tanzania ndiyo ikaamua kulituma shirika la ndege la Taifa Air Tanzania Corporation (ATC) kwenda kuchukua mwili wa Mwl. Nyerere na ndege yetu aina ya Boeing 737 – 300 ambayo tulikuwa tume lease kutoka kampuni ya ANSETT ya Australia, lakini ilikuwa na bendera ya Tanzania na marubani na mafundi pamoja na wahudumu walikuwa watanzania. Ilisaidia kujenga heshima ya kitaifa mbele ya Mataifa yaliokuwa yakifuatilia mazishi hayo. Shirika letu la ndege la Taifa lilimudu jukumu hilo kwa ufanisi mzuri ( NATIONAL FLAG CARRIER) na kuuleta mwili wa mwalimu bila tatizo lolote, na mwili huo ulibebwa na askari wa Royal family hadi ndani ya ndege yetu ya ATC. Pia mwili wa marehemu Mwl. Nyerere ulibebwa na ndege ya serikali aina ya FOKKER 50 hadi Musoma kwa safari ya mwisho ya mwalimu kwa ajili ya mazishi.

Mbowe abwagwa Mahakamani, atakiwa kulipa sh. bil. 1.7 kurudishiwa vitu vyake
Jaji aliyesikiliza kesi ya bilionea wa dawa za kulevya ‘El Chapo’ auawa