Kutokana na matukio ya vitendo vya ugaidi, uharamia na madawa ya kulevya yamechangia Wanajeshi wa Tanzania kwa ushirikiano wa serikali ya nchi  na Jeshi la Marekani na kuzihusisha nchi nyingine za Afrika Mashariki pamoja na Taasisi za Umoja wa Afrika.

Hali hiyo pia imechangia majukumu ya majeshi ya nchi mbalimbali kuanza kubadilika na kutolewa kwa mafunzo yanayowapa uwezo wanajeshi wa nchi mbalimbali kuweza kupambana na uhalifu huo.

Waziri wa Ulinzi wa Tanzania Dokta Hussein Mwinyi amesema matukio ya uharamia ama ugaidi hayana mipaka na hivyo ni lazima yakapigwa vita kwa pamoja, akisisitizia umuhimu wa kuwepo kwa mafunzo kama hayo.

Ushirikiano wa pamoja wa kijeshi pia umechangia kusaidia kumaliza matukio ya uharamia katika bahari kuu yaliyoathiri nchi jirani ikiwemo Tanzania kutokana na kutokuwepo kwa serikali dhabiti nchini Somalia.

Mafunzo hayo yaliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam yakizishirikisha nchi za Uingereza na Ujerumani pamoja na Shirika la Kimataifa la RedCross.

Polisi wasusa kulinda baada ya wachezaji kuvaa fulana kuhusu Weusi waliouawa
Video: Mabigwa wa Euro 2016 Walivyopokelewa Lisbon