Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Ruvuma, limekusanya Sh bilioni 1.3 katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba 2020 kutokana na makosa ya mbalimbali ya barabarani.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Pili Mande ameeleza kuwa katika kipindi hicho, magari 46,598  yalikamatwa na kikosi hicho yakiwa na makosa mbalimbali Kamanda huyo amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema katika kipindi hicho, kulitokea ajali 39 ambapo 27 zilisababisha vifo vya watu 42, kati yao wanaume 6 wanawake 36. Ajali zilizosababisha majeruhi zilikuwa 12 na hizo zilisababisha majeraha kwa watu 57.

Aidha, Kamanda Mande amesema watuhumiwa 21 walikamatwa wakiwa na nyara za serikali, ambazo ni miguu miwili na utumbo wa nyati, vipande 30 vya vyama ya kuro, vipande 26 vya ngorombwe, vipande 21 vya nyama ya tembo na vipande 25 nyama ya nguruwe pori.

Kamanda Mande amesema walikamata watuhumiwa wawili wakiwa na silaha mbili, ambazo ni shotgun moja na gobole. Pia walikamata watu watatu wakiwa na mali ya wizi, ambayo ni mafuta ya dizeli lita120 na mafuta ya kula aina ya Oleo Miaia ndoo 178 za lita kumi.

Tambwe achimba 'MKWARA' mzito Young Africans
Onyo kwa vyuo binafsi vya Famasi