Mwamba wa Kaskazini, Joh Makini amesema kuwa tangu aanze muziki hajawahi kuishi kwenye bifu na msanii yoyote, tofauti na tetesi nyingi zilizowahi kuingia mitaani.

Joh Makini amefunguka leo kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio alipoulizwa na mmoja kati ya mashabiki wake aliyetaka kujua kama ni kweli ana bifu na rapa mwenzake toka Mwanza.

“Inaonekana washkaji mkiwa kitaa mnatengeneza movies za bifu eeh… tangu nianze muziki sijawahi kuwa na bifu na mtu yoyote,” amefunguka.

“Hii ni kwa sababu naamini kuwa muziki wangu unaweza kukua na kuwa na maendeleo ninayoyataka bila kutengeneza bifu na yeyote,” alifafanua.

Rapa huyo wa kundi la Weusi ambaye alipata umaarufu kupitia mashairi ya tambo na majigambo, hivi karibuni alikanusha taarifa zilizosambazwa kuwa ana bifu na Nahreel wa Navy Kenzo, taarifa ambazo pia zilikanushwa na Navy Kenzo.

Live kutoka Ikulu: Ziara ya Mfalme wa Morocco, Mohamed VI nchini Tanzania
Video: Waziri Mwijage asema watanzania wanapenda elimu 'mserereko', Azungumzia elimu yake