Kampuni ya Johnson & Johnson ya Afrika Kusini inatarajia kuondoa mauzo ya poda yake aina ya TALC Baby Powder mwaka 2023.

Poda hiyo ambayo imesimama kuuzwa Nchini Marekani na Canada kuanzia mwaka 2020, imekua na kesi maelfu juu ya kusababisha matatizo ya kansa ya ovari kwa wanawake walioitumia kwa muda mrefu.

Kampuni huyo imeendelea kusema kuwa suala hilo litabakia kuwa siri ya ndani ya Kampuni kwa usalama wa bidhaa nyingine lakini imetangaza kuacha kuisambaza duniani kote poda hiyo yenye kiungo cha Talc kwa sababu za kufanyiwa uchunguzi.

Baadhi za Tafiti za kisayansi zimeonesha kuwa kiungo cha Talc kimekuwa kikisababisha Kansa kwa wanawake wanaoutumia katika sehemu za uke, na Kampuni nyingi zenye kutengeneza bidhaa za kiungo hicho zimekuwa zikiweka alama ya hatari katika bidhaa hizo lakini kampuni ya JNJ imekua ikisema kuwa lebo hiyo italeta mkanganyiko kwa watumiaji.

Jopo la majaji wa St. Louis jury walifikisha Oda ya Deni la Dola billion 4.7 kwa Kampuni hiyo mwaka 2018 likisema kuwa Kampuni hiyo imekataa kweka onyo kwenye bidhaa hiyo ili kuwalinda wateja na hatari.

“Msimamo wetu kama Kampuni kuhusu usalama wa bidhaa za Talc Poda haubadiliki, kwa sababu kwa miaka kadhaa wataalamu wamekuwa wakipima bidhaa hii na hawakusema kama inasababisha matatizo ya afya kwa watumiaji.” Imesema Kampuni hiyo.

‘Johnson’s baby powder’ imekuwa katika mauzo tangu mwaka 1894 na ilibaki kama alama nzuri ya biashara ya Kampuni na picha nzuri kwa familia.

Kenya: Familia ya Oginga yangojea matokeo ya Odinga kwa hamu
Basi la New Force lauwa mmoja sita majeruhi