Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amemteua Mhandisi Emmanuel Korosso kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ndege Tanzania(ATCL) kwa miaka mitatu, ambapo kabla ya kuteuliwa Mhandisi  Korosso alikuwa  Meneja TANROADS Musoma.

Akitoa taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Dk. Leonard Chamuriho amesema pamoja na uteuzi huo Rais  Magufuli amemteua Mhandisi Ladislaus Evarist Matindi kuwa Mkurugenzi mpya wa ATCL ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Africa Joint Programme (EGNOS) akishughulikia masuala ya Anga katika Ukanda wa Afrika.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa ameteua Wajumbe wa Bodi watano ambao ni Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye amebobea katika Menejimenti ya Kimataifa na  Utawala Bora wa Bodi na Taasisi za Kifedha, Dk. Neema Mori Munishi, Mkurugenzi wa Utalii na Masoko ambaye anafanya kazi TANAPA, Ibrahim Mussa, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu

Mambo 10 ya kufanya kabla hujafikia miaka 28
Magufuli aipangua TTCL, amuondoa Mtendaji Mkuu na kumteua Kindamba