Meneja wa majogoo wa jiji Liverpool Jurgen Klopp amemtaja David Silva wa klabu ya Man City kama mchezaji pekee katika Ligi ya kuu wa Uingereza anaemvutia kwa kiasi kikubwa.

Akiongea katika kipindi cha Sky Sports’ ‘Monday Night Football’, Klopp ameweka wazi mapenzi yake kwa mchezaji huyo kutokana na aina ya uchezaji wake.

“Nampenda sana David Silva, ni mchezaji wa aina yake, anazunguka uwanja mzima, ni ana akili nyingi akiwa uwanjani pamoja na mtazamo chanya muda wote,”

“Hata kama sijasikia jina lake likitamkwa sana kufuatia mwanzo mzuri wa klabu yake ya Man City kwenye msimu huu wa Ligi ya Uingereza, lakini nina uhakika kabisa kazi yake inaonekana na napenda sana ain yake ya uchezaji.”

“Lakini hata hivyo sivutiwi sana na wachezaji wa timu nyingine kwani wana hatari kubwa pale unapokutana nao.” Alisema Klopp

Klopp ameanza vizuri msimu huu akiwa na kikosi cha Liverpool ambacho kimeshinda michezo minne ikiwemo dhidi ya Arsenal na Chelse ugenini, ametoa sare mara moja na kufungwa mchezo mmoja.

Dangote: Mimi ni mzima na buheri wa afya, alikanusha kauli iliyosema amefariki dunia
Majimaji FC Wamrejesha Kally Ongala