Justin Bieber amerusha mapigo kwa mitandao maarufu ya Marekani iliyoandika habari inayomnukuu akitoa maelezo ambayo mitandao hiyo ilidai anajifananisha na Mungu.

Jana, Mwimbaji huyo ambaye yuko kwenye ziara yake ya dunia aliyoipa jina la ‘Purpose World Tour’ alipost picha akiwa kifua wazi amejilaza kitandani na kuandika maelezo yanayonukuu kifungu cha Biblia Takatifu kinachoeleza kuwa Siku ya Saba Mungu alipumzika baada ya kufanya kazi kwa siku sita.

Mitandao hiyo ikiwemo Hollywood Life ilieleza kuwa Bieber ameingia kwenye mkumbo wa Mastaa wengi wakubwa nchini humo wa kujifananisha na Mungu.

Leo, Bieber amerudi kwenye ukurasa wake wa Instagram kujibu tuhuma hizo akiambatanisha na picha inayoonesha vipande vya tovuti zilizoandika taarifa hiyo.

“Napenda kuzungumza kwa sababu ni wakati mwingine wa kumnyooshea Mungu. Niliposema siku ya saba ilikuwa kunukuu kwamba katika siku ya 7 [Mungu] alipumzika inatupa mfano wa kufahamu namna ambavyo mapumziko ni muhimu. Watu wanapenda kubadili mambo, kilichomaanishwa kwa wema au labda ilikuwa kosa langu kwa kushindwa kuelezea mawazo yangu kwa usahihi. Unaweza kufikiria mabaya yote kuhusu mimi lakini staki hata kidogo watu wafikirie kwamba nilijifananisha na Aliye Juu,” Inasomeka Post ya Bieber kwa tafsiri iliyofanywa kwa hisani ya Dar24. Hii ni post nyingine ya Bieber kuhusu sakata hilo;

Utafiti: Wananchi hawapendi serikali kufungia magazeti kwa mtindo huu
Ray Parlour: Diego Simeone Anafaa Kuwa Meneja Wa Arsenal