Sakata la ufisadi wa mabilioni kupitia Benki ya Stanbic limewafikisha mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Dk. Harry Kitilya na aliyekuwa Miss Tanzania 1996, Shose Sinare pamoja na mwenzao Sioi Solomoni.

Watatu hao wametinga leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka matatu yanayohusiana na ufisadi huo unaodaiwa kufanyika Machi mwaka 2013.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuhusika katika uuzwaji wa hati fungani za serikali kupitia Benki ya Stanbic tawi la Tanzania.

Mwishoni mwa mwaka jana, ripoti za uchunguzi za awali zilizofanywa na Taasisi ya Makosa Makubwa ya Ufisadi ya Uingereza (SFO) ulibaini kuwa watuhumiwa hao waliomba kupewa shilingi bilioni 13 ili kufanikisha mkopo huo wa shilingi trilioni 1.3 huku wakitumia njia nyingi za ‘ujanjaujanja’ kinyume na sheria.

Hata hivyo, watuhumiwa wote walikana mashtaka na kurudishwa rumane hadi Aprili 8 mwaka huu kesi yao itakaposikilizwa tena.

Makonda awageukia Bodaboda, awaahidi pikipiki kwa Sh 3,500 kwa siku, kuingia posta
Ferguson: Ni Ndoto Kwa Man City Kucheza Kama FC Barcelona