Kanye west “YE” amefunguka kuhusu mahusiano yake na rapa Beg sean ambaye alikuwa chini yake kupitia Good Music Record Label, Kanye ameendelea kudhihirisha kuwa yeye na Big Sean kwa sasa hali yao kimaelewano ni tete ambapo kupitia kwenye mahojiano aliyofanya na Drink Champs kupitia Revolttv, amesema kitendo cha yeye kumsaini rapa Big Sean kwenye Lebal yake ni kitu kibaya zaidi ambacho amewahi kufanya kwenye maisha yake.

Mara baada ya kujitoa kwenye Label ya Kanye, Wiki chache zilizopita rapa Big Sean alitangaza rasmi kufungua Label yake mpya iitwayo ‘FF to Def Entertainment’ ambayo mpaka sasa tayari imekwisha anza kufanya kazi, kwa madai ya kuwa ni bora kumiliki kilicho chake kwa kuwa Kanye West hakuwahi kumlipa Pesa zake licha ya kutengeneza nyimbo nyingi zilizofanikiwa kufanya vizuri sokoni kwa kipindi kirefu tangu kujiunga kwake na Label hiyo.

Kanye West na Big Sean bifu lanukia.
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 5, 2021