Polisi nchini Marekani wanamchunguza Kanye West kwa tuhuma za kumpiga mtu mmoja aliyekuwa akimfuata akihitaji sahihi ama ‘Autograph’ ya msanii huyo, wakati ambao Kanye hakuwa tayari kwa hilo.

Shambulio hilo linadaiwa kufanyika majira ya saa 9 usiku huko DTLA, nje ya Soho Warehouse, huku mashuda wakibainisha kuwa Ye alionekana kuwa mwenye hasira sana.

Kwa mujibu wa TMZ ambao walifanikiwa kunasa kipande kidogo cha Video kinachoonyesha tukio lilivyokuwa, inamuonyesha Kanye akipiga kelele, huku akitamka maneno yaliyosikika “ondoka kwangu” akimwambia mwanamke ambaye alikuwa akijaribu kumtuliza baada ya tukio hilo huku mwanamke huyo ambaye inadaiwa kuwa ni binamu yake akimjibu Kanye kwa kusema, “Mimi ni familia yako,” lakini bado Ye aliendelea kuruka kwa hasira.

Mashahidi wamesema kuwa tukio la kurushiana maneno na mwanamke huyo,  limetokea sekunde chache tu baada ya Kanye kudaiwa kumpiga kijana huyo ngumi mbili, moja kichwani, na moja shingoni, na kuanguka chini huku kichwa chake kikijipiga chini kwa nguvu.

Inadaiwa Kanye alikuwa amewataka watu wachache waliokuwa nje ya jengo hilo kutopiga picha na kudokeza kuhusu wao kutoelewa anachopitia hivi sasa.

Mtu alipojibu kuwa ni sawa sote tunapitia mambo ya kifamilia ndipo Kanye alikasirika na kuamua kushusha ngumi mbili.

Inaelezwa Kanye alikuwa anaelekea katikati mwa jiji baada ya kutoka kurekodi usiku wa manane katika studio za  ‘Hollywood’.

Mtuhumiwa alikataa matibabu katika eneo la tukio, lakini inaelezwa kuwa kwa sasa anapatiwa huduma ya dharura huku Kanye west akifanyiwa uchunguzi wa kina.

Hii sio mara ya kwanza kwa Kanye West kupatwa na hatia ya makosa ya namna hiyo, tukio la kwanza alilifanya mnamo Machi 2014, dhidi ya mpiga picha ambaye alimshtaki kwa kosa la kumfsnyia fujo na kumharibia vifaa vyake.

Wakati huo kanye West alitakiwa kupitia vikao takribani 24 vya kudhibiti hasira, pamoja na kazi za jamii kwa muda wa masaa 250 kama adhabu ikiwa ni pamoja na kumlipa fidia  muathirika wa tukio hilo.

Polisi wa Beverly Hills pia walichunguza tukio la Januari 2014 ambapo West alishutumiwa kwa kumpiga mwanamume mmoja katika ofisi ya tabibu, ambapo Kanye alifikia makubaliano ya kawaida na mtu huyo na kisha kuyamaliza kimya kimya.

Talibani yaitaka Marekani kuachia fedha zake
Rc Hapi: Serikali haijarejesha ada