Kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole imegeuka kuwa kitendawili cha aina yake, wakati ambapo Rais John Pombe Magufuli amewaondoa viongozi mbalimbali Serikalini baada ya kuchukua fomu kugombea ubunge.

Akizungumza jana, Julai 18, 2020 kwenye mkutano wa ndani Mkoani Ruvuma, kuhusu utekelezaji wa Ilani ya CCM, Polepole amewataka viongozi kutosheka na nafasi walizonazo na kuzingatia nidhamu.

Hii ndiyo kauli ya Polepole iliyogeuka kitendawili. Unaweza kusaidia kukitegua, au kama ni fumbo unaweza kusaidia kulifumbua kwa kuzingatia mazingira ya kuelekea Oktoba, 2020 kwenye Uchaguzi Mkuu.

“Mwaka 2015, Rais Magufuli alipovuka akawaambia baadhi ya watu ‘hallo, wewe njoo, naona kama umekwama hivi lakini naona unaweza kutufaa kwenye chama chetu, hebu shika nafasi hii, nisaidie kwa jukumu hili. Kule mbele kuna mto, mimi kuogelea siwezi [nakupa mfano]. Tukifika pale, chapa hii kazi utanivusha pale utanivusha kwenye ule mtu,”

“Basi unakuwa unakula vinono vya mzee Magufuli mnakula tu wewe na mkeo mnakula tu… mnafika mtoni unasema ‘mzee mimi nimegaili siendi, kama ni kuvuka vuka mwenyewe’ haah! Si ni ulaghai huu!? Ingekuwa kule Pwani ningewaimbia, ‘mahindi yangu umekula, soda yangu umekunywa, haiwezekani uondoke hivi-hivi.”

“Sasa mimi nawapongeza sana safu yako ya Mkoa [Ruvuma], ninyi Mungu amewasaidia mmeona mbele. Kwa sababu chama hiki kikipata viongozi wasiotosheka ni shida. Hawataaminika popote. Mtu asiyetosheka, ukimpa kazi hii atakuacha mtoni atachukua nyingine, na ukimpa hiyo hatatosheka atakuacha mtoni,”

“Sasa haya mambo ya kuachana mtoni Mwenyekiti ametusaidia, anaanza kuiweka sawa. Wewe si unakwenda bana, tuachie mambo yetu uende. Na sasa tukija kwenye chama kule… nisiwaambie lakini kwakweli… [anacheka]. Tutakuwa…. ‘alituvusha kwenye mto hakutuvusha huyu? Aah, alitukimbia mtoni. Basi tufanye tu utaratibu wa kumsaidia huyu, mtu aliyekukimbia mtoni, wewe vuka mwenyewe. Umuache hukohuko aliko. Nidhamu… tukiharibikiwa kwenye nidhamu tumeliwa.”

Waziri Mkuu ahimiza kilimo cha mboga Ruangwa

Kubenea ahamia ACT – Wazalendo

Rwanda yawanasa magaidi 57, wasombwa kutoka msituni
Waziri Mkuu ahimiza kilimo cha mboga Ruangwa