Wakati wakenya wakiendelea kusubiri matokeo kwa nafasi ya Urais, Tume huru ya mipaka na uchaguzi nchini Kenya IEBC imetangaza kuondolewa kwa kura 10, 000 kutoka hesabu ya William Ruto.

Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati, amesema kuna kura 10, 000 DP Ruto alipata kimakosa katika kaunti ya Kiambu.

Kwa mujibu wa ripoti ya IEBC, Ruto alikuwa ameorodheshwa kupata kura 51050 katika eneo la bunge la Kiambu katika Fomu 34B badala ya 41050.

“Ni kosa ambalo lilitambuliwa wakati wa kujumuishwa kwa kura na likarekebsishwa mara moja.” Chebukati.

Hata hivyo taarifa za uwepo wa wizi wa kura zimeendelea kusambaa ambapo umakini kwa sasa umeelekezwa katika Kituo cha Bomas.

Washirika wa Azimio la Umoja wamedai takwimu zinaonesha kuna idadi nyingi ya kura zilizopigwa nafasi ya Urais kuliko Wagombea wa nafasi nyingine na asilimia kubwa matukio hayo yamefanyika katika vituo alivyopigiwa kura nyingi mgombea wa UDA, William Ruto.

Katibu wa Chama cha Jubilee, Jeremiah Kioni ambaye wanamuunga mkono Raila Odinga amesema idadi ya kura katika vifaa vya KIEMS hailingani na idadi ya wapiga kura inayoonekana kwenye Makaratasi.

Serikali yatoa taarifa mwenendo wa Uviko-19
Kenya: Washona wapiga kura kwa mara ya kwanza tangu 1960