Serikali ya Kenya imesema kuwa itawalipa fidia wafugaji kutoka familia kumi kutoka Kaunti ya Kajiado ambao mifugo yao iliyotaifishwa na Serikali ya Tanzania na kupigwa mnada baada ya kuvuka mpaka bila kufuata utaratibu.

Imesema kuwa imetenga zaidi ya Ksh. 55 M kuwawezesha wafugaji hao kununua ng’ombe wengine, huku juhudi za kuutatua mgogoro wa Kidiplomasia unaendelea kati ya Kenya na Tanzania zikishika kasi.

Aidha, siku za hivi karibuni, Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania, Luhaga Mpina alifanya ziara mkoani Kilimanjaro na kukuta kundi kubwa zaidi ya ng’ombe 6000 zilizokuwa zimevuka mpaka bila kufuata utaratibu.

Hata hivyo, baada ya kukamatwa kwa ng’ombe wamiliki walikimbia na kuzitelekeza, hivyo kuamuliwa kufuatwa taratibu za kimahakama ili ng’ombe hao wapigwe mnada.

Video: Dk. Slaa aajiriwa Supermarket, Mbowe aibua upya sakata la Lissu bungeni
ACT- Wazalendo wadai kuhujumiwa