Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amemtangaza Dkt William Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais kwa kupata kura 7,176 141, ikiwa ni asilimia 50.49 ya kura zote halali.

Kiongozi wa Azimio Raila Odinga anashika nafasi ya pili kwa kura 6,942, 930, akiwakilisha asilimia 48.85 ya kura zote halali, huku William Ruto, akitoa hotuba yake baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais.

Amesema, “Kulikuwa na utabiri kwamba hatutafika hapa. Lakini kwa sababu kuna Mungu mbinguni, tulifika hapa na sasa nawashukuru Wakenya kwa kuepuka ukabila na leo nawaambia Mungu yupo na ushindi huu ni wa Wakenya wote.”

Aidha, Ruto amemshukuru mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, Wafula Chebukati kwa kuweka matokeo ya uchaguzi kwenye tovuti ya umma, na kufanya kuwa ya uwazi na ukweli ambayo yameandika historia kwa wakenya.

Amefafanua kuwa “Shujaa wa uchaguzi huu ni IEBC, inayoongozwa na Wafula Chebukati, ninataka kuishukuru IEBC kwa kuinua kiwango hicho na ninawashukuru wakenya wote ninawaomba ushirikiano ili kuifikisha Kenya mbele na hakuna kurudi nyuma tufanye kazi pamoja asante.”

Katika hatua nyingine, Ruto amemshukuru Rais anayeondoka madarakani Uhuru Kenyatta, na kuahidi kujenga misingi ya utawala alioachiwa na Uhuru huku akiahidi kufanya kazi na viongozi wote waliochaguliwa na kusema atafanya kazi na upinzani na watatoa uangalizi katika utawala wake.

Ligi Kuu ya NBC kuendelea leo
Ruzuku yawakutanisha pamoja Wadau wa AZAKI