Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres amewapongeza Wananchi wa Kenya kwa kupiga kura kwa amani wakati wa Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Agosti 9, 2022.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu wa UN, Stéphane Dujarric jijini New York, Marekani imesema Guterres anatambua kazi muhimu iliyofanywa na mamlaka ya Kenya pamoja na mashirika mengi yote yanayohusika na usimamizi wa uchaguzi.

Amesema, ushirikishwaji wa wadau mbalimbali wa kitaifa na dhamira ya dhati isiyoyumbishwa ya wapiga kura kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kuwataka Wananchi hao kuendelea kuwa watulivu wakati tume ikifanya majumuisho ya matokeo ya kura.

“Katibu Mkuu ana imani wadau wote wa kisisasa na wananchi wa Kenya wataendelea kuonesha kiwango hicho hicho cha utulivu, Subira na heshima kwa mchakato huo wa uchaguzi wakati huu wakisubiri kutangazwa kwa matokeo ya kura kwa mujibu wa muda uliowekwa kisheria,” amesema Dujarric.

Hata hivyo, Guterres amesisitiza uwepo wa Umoja wa Mataifa na kuendelea kuunga mkono juhudi zote zinazofanywa na mamlaka ya nchi hiyo kwa kuwahusisha Wananchi wote wa ili kuhakikisha wanaendeleza mchakato wa kidemokrasia nchini humo.

Muliro: Marufuku mashabiki kwenda na silaha kwa Mkapa
Kocha Azam FC atuma salamu Ligi Kuu Bara