Wagombea wa kiti cha Urais Kenya akiwemo William Ruto wamewasili katika ukumbi wa Bomas ambao matokeo ya urais yatatangazwa na Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, Wafula Chebukati.

Ruto amewasili hapo kwa nyakati tofauti akiongozana na mama yake Sarah Cheruiyot, aliyepishana naye muda mchache kuwasili hapo ili kuja kushuhudia iwapo mwanaye atashinda kiti cha urais dhidi ya mgombea Azimio la Umoja, Raila Odinga aliyekuwa akichuana naye vikali ambaye naye amewasili katika ukumbi huo.

Waihiga Mwaure (kulia) na George Wajackoyah (Kushoto) wakiwasili Bomas kusikiliza matokeo. Picha na Dennis Onsongo/NMG

Wgombea wengine waliowasili ni pamoja na Chama cha Agano, Waihiga Mwaure na George Wajackoyah wa chama cha Roots party.

Takwimu sensa kusaidia tathmini za Wafanyabiashara
Mafuriko yauwa 31, wengi ni Wanawake na Watoto