Chama cha wasioamini Mungu nchini Kenya (AK) kimemtaka Mhubiri David Owuor, kumfufua aliyekuwa waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi, Jenerali Joseph Nkaissery.

Ombi hilo wamelitoa baada ya kuvuma taarifa kuwa, mihubiri huyo alimfufua mwanamke aliyekuwa amefariki dunia katika kaunti ya pokot Magharibi, wiki iliyopita.

Kwenye ujumbe uliochapishwa katika tovuti ya chama hicho cha wasiomwamini Mungu (AK), kimedai kwamba ikiwa ni kweli mhubiri huyo ana uwezo wa kukufua, basi anapaswa kumfufua Nakissery ili aendelee kuihudumia nchi.

”Ikiwa ni kweli kwamba Owuor alimfufua mtu kimuujiza, basi tunaomba akamfufue Nakissery kutokana an mchango wake mkubea nchini” wamesema waumini wasioamini uwepo wa Mungu.

Kutokana na madai hayo waumini wa kanisa la Repentance wamekuwa wakifanya maandamano ya kusherekea muujiza huo kila jumapili.

Sherehe hizo zimekuwa zikifanyika kila jumapili katika baadhi ya miji mikubwa ikiwemo Nairobi na Eldoret.

 

DCI amsaka aliyesambaza video mchele wa plastiki
Afande Sele: Ofisi ya chama cha soka Tanzania aibu yetu