Mahakama ya mjini Instanbul imeanza vikao vya kusikiliza kesi inayohusu mauaji ya mwaka wa 2018 ya mwanahabari mkosoaji wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi. 

Kesi ya washitakiwa 26 wa mauaji hayo iliyofunguliwa Julai mwaka jana inaendelea bila wao kuwepo mahakamani. 

Saudi Arabia ilikataa kuwahamishia Uturuki washukiwa hao, ambao wanamjumuisha Ahmed al-Asiri ambaye alikuwa Naibu Mkuu wa ujasusi, na Saud al-Qahtani, mshauri wa zamani wa mrithi wa kiti cha Ufalme Mohamed bin Salman. 

Inadaiwa Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi wa Saudia mjini Instabul mnamo Oktoba 2, 2018.

Kwa mujibu wa mashitaka ya Uturuki, Khashoggi alinyongwa hadi kufa na mwili wake kukatwakatwa vipande.

 Mabaki ya mwandishi huyo wa gazeti la Washington Post la Marekani ambaye wakati mmoja alikuwa mtu wa karibu na familia ya Kifalme lakini akageuka kuwa mkosoaji mkubwa wa mwanamfalme, hayakuwahi kupatikana.

Simba SC wafurahia mapokezi Khartoum
Serengeti Boys safarini Morocco