Wanafunzi wa Kidato cha Sita hii leo wanatarajiwa kuanza mitihani yao ya Kitaifa ambayo itawapelekea kumaliza elimu ya Sekondari hapo mwisho wa mitihani hiyo Mei 27.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde amesema kuna jumla ya watahiniwa Elfu 95, mia tisa na 55 kutoka shule za sekondari 841 na vituo vya kujitegemea 250.

Pia watahiniwa 9,670 kutoka vyuo 70 wamesajiliwa kufanya mitihani ya mwisho ya kozi ya ualimu katika ngazi ya stashahada na cheti.

Dk Msonde amesema kati ya watahiniwa wa kidato cha sita 85,531 ni wale wa shule na 10,424 ni wa kujitegemea.

“Kati ya hao wanaume ni 47,859 ni wavulana sawa na asilimia 55.96 na wasichana ni 37,672 sawa na asilimia 44.04,” amesema Dk Msonde.

“Pia watahiniwa wenye mahitaji maalumu wapo 151 na kati yao 136 ni wenye uoni hafifu na 15 ni wasioona.”

Kati ya watahiniwa wa kujitegemea 10,424 waliojisajili, wanaume ni 6,546 sawa na asilimia 62.80 na wanawake ni 3,878 sawa ana silimia 37.20 na asiyeona ni mmoja.

Kati ya walimu wataketi kufanya mtihani huo, 4,560 ni ngazi ta stashahada na 5,110 ni ngazi cheti.

Dk Msonde amesema baraza halitasita kukifuta kituo chochote cha mitihani endapo litajiridhisha kuwa uwepo wake unahatarisha usalama wa mitihani ya Taifa.

Msonde amewataka Mwalimu wake kutoingilia kazi za wasaimamizi wa mitihani hiyo kwani shule ni vituo maalumu vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote cha ufanyaji mitihani.

Habari kubwa kwenye Magazeti leo Mei 9, 2022
Breaking:Rais Samia aitisha kikao usiku kujadili bei ya Mafuta