Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Khamisi Kigwangalla amelaani kitendo cha Gardner G. Habash kutoa maneno ya udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mkewe, Lady Jay Dee.

Kumekuwa na kipande cha video kilichosambaa mitandaoni kinachomuonesha Gardner akiwa katika jukwaa moja hivi karibuni, ambapo alitoa kauli za udhalilishaji. Ingawa hakumtaja jina, maelezo na wimbo wa mpya wa Jide uliopigwa mwishoni mwa kauli yake ‘Ndindindi’ vilijieleza.

Kigwangalla Tweets

Kigwangalla ametumia mtandao wa Twitter kukemea kauli alizotoa Gardner na kumtaka aombe radhi pamoja na mwajiri wake Clouds Media Group.

Tani 622.4 za sukari zakamatwa mkoani Morogoro
Sitta awatetea wabunge wa Chadema

Comments

comments