Jeshi la Polisi Mkoani Kagera linamshikilia Ayoub John (38) ambaye ni mvuvi katika kisiwa cha Chakazibwe wilaya ya Muleba kwa tuhuma za kumchinja mtoto wake wa kambo Aidan Greyson (3).

Kamanda wa polisi mkoani humo Revocatus Malimi amesema kuwa mtoto huyo wa kiume anadaiwa kuuwawa na baba yake wa kambo usiku wa kuamkia agosti 8, mwaka huu ambapo chanzo cha mauaji hayo ni kuzuka kwa ugomvi baina ya John na mkewe Mektirida Nestory (27)

”kulizuka ugomvi mkubwa kati ya wanandoa hawa na baada ya baba kurudi nyumbani alikuwa amelewa walipigana na mama akaamua kukimbilia kwa jirani na kumuacha mtoto huyo aliyezaa na baba mwingine kabla ya kuolewa na mtuhumiwa aliporejea asubuhi alikuta mtoto ameuawa” amesema Kamanda Malimi

Sambamba na hilo Kamanda Malimi amesema Jeshi linawasaka watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Rwegoshora Lonce (55) kwa kumpiga na silaha za jadi ikiwemo fimbo baada ya kumtuhumu kuiba mkungu wa ndizi wenye thamani ya shilingi 50,000.

Amesema watuhumiwa hao baada ya kumpiga walimpeleka kwa mwenyekiti wa kitongoji cha kakiriusiku wa saa tano agosti 7, 2020 na baadae kumpeleka kwa mjomba wake na kumtelekeza huko ambapo kesho yake alifariki dunia.

Wachezaji 10 ruhsa Ligi Kuu
Simba SC yawaita Young Africans mezani

Comments

comments